China na Togo zatazamia ushirikiano wa karibu zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2024

Rais wa Togo Faure Gnassingbe (Kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Lome, Togo, Januari 17, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Rais wa Togo Faure Gnassingbe (Kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Lome, Togo, Januari 17, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

LOME - Rais wa Togo Faure Gnassingbe siku ya Jumatano alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Togo, huku pande zote mbili zikieleza nia ya kuongeza uhusiano wao na kuendeleza ushirikiano kati ya Afrika na China.

Rais Gnassingbe amemuomba Wang kuwasilisha salamu zake za dhati na za kutakia kheri kwa Rais Xi Jinping wa China na kupongeza sana uhusiano na ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili.

Chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, Togo na nchi nyingine za Afrika zimepata maendeleo katika ujenzi wa miundombinu, Gnassingbe amesema.

Afrika imeongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake, kuimarisha usalama na kuleta manufaa kwa watu wa bara hilo, amesema Rais Gnassingbe, huku akisisitiza kuwa mafanikio haya yasingeweza kupatikana bila msaada wa muda mrefu na wa kujitolea wa China.

“Togo inashukuru China kwa kushikilia haki katika jukwaa la kimataifa, kupinga uingiliaji kati masuala ya ndani ya Afrika, na kutoa mchango muhimu katika maendeleo ya amani ya Afrika,” rais amesema.

Amesema, watu wa Afrika wanahitaji rafiki kama China, ambaye anajali hali halisi ya Afrika, anasikiliza matakwa ya Afrika, na kamwe halazimishi matakwa yake kwa wengine.

Kwa upande wake Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amewasilisha salamu kutoka kwa Rais Xi Jinping. Amesema kuwa, urafiki kati ya China na Togo, ulioanzishwa na viongozi wa kizazi cha zamani, umekuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Amesema China itaimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo na Togo na kuiunga mkono Togo katika kufikia maendeleo endelevu.

Amesema China inaelewa na kuiamini Afrika, huku akibainisha kuwa maadam Afrika ina umoja na uhuru, inaimarika kupitia umoja, na kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali ya taifa, itaweza kushinda changamoto na kuunda fursa mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha