

Lugha Nyingine
Mambo yanayohusiana na China yang'ara katika AFCON 2023
Picha iliyopigwa tarehe 8, Januari ikionesha Uwanja wa Alassane Ouattara, ambao unajulikana kama Uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe mjini Abidjan, Mji Mkuu wa kiuchumi wa Cote d'Ivoire. (Picha/IC Photo)
Tarehe 13, Mashindano ya 34 ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yalifunguliwa nchini Cote d'Ivoire. Michezo hiyo hudumu kwa karibu mwezi mzima, na itafanyika kwenye viwanja sita katika miji mitano ya Abidjan, Bouake, Yamoussoukro, Korhogo na San-Pedro. Kati ya viwanja hivyo, Uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe mjini Abidjan, Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro na Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo vilijengwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la Beijing, Shirika la CRCC la China na Shirika la CNBM la China.
“Tunayo furaha kwa ushirikiano kati ya Cote d'Ivoire na China. Huu ni mfano wa ushirikiano, na uwanja huu ni uthibitisho bora,” amesema mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya AFCON ya Cote d'Ivoire Francois Albert Amichia kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe.
Picha iliyopigwa tarehe 9, Januari ikionesha mandhari ya uwanja wa michezo na mji mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. (Picha na Han Xu/Xinhua)
Natara ni msichana aliyezaliwa kwa baba na mama wenye asili ya nchi mbili tofauti za Nigeria na Cote d'Ivoire aliyezaliwa nchini Nigeria. Baada ya kurudi Cote d'Ivoire, alijifunza lugha ya Kichina na kujiunga na Shirika la CNBM la China, akiwa mkalimani wa mafundi waliojenga mradi wa uwanja mjini Korhogo.
“Baada ya kurudi Cote d'Ivoire, nilishangazwa na maendeleo nchi hiyo iliyoyapata, na sehemu kubwa miundombinu yake imejengwa na kampuni za China, kwa hivyo niliamua kujiunga nao na kujenga mji wangu pamoja nao," amesema Natara.
Picha iliyopigwa tarehe 13, Januari ikionesha Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro, Cote d'Ivoire. (Picha na Dai He/Xinhua)
Usiku wa tarehe 13 saa 2 kwa saa za Cote d'Ivoire, katika Kijiji cha Yaou kilichopo umbali wa kilomita zaidi ya 40 Mashariki ya Abidjan, makumi ya wanakijiji walikuwa wamekaa kwenye chumba cha shughuli cha kijiji hicho kwa ajili ya kutazama mechi ya kwanza ya mashindano ya AFCON ya mwaka huu, ambayo ilikuwa ni kati ya Cote d'Ivoire na Guinea-Bissau.
Watu wakitazama mechi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwa usaidizi wa mradi wa TV wa satelaiti wa China katika Kijiji cha Yaou, Cote d'Ivoire, Januari 14, 2024. (Xinhua/Han Xu)
“Shukrani kwa StarTimes kwa kuunganisha kijiji chetu na mawimbi ya televisheni za satelaiti, hatimaye tunaweza kukaa pamoja kama familia na kutazama mechi za soka!” amesema mwankijiji.
Asubuhi ya tarehe 14, Januari, kwenye mechi ya kirafiki kati ya wakongwe wa soka iliyofanyika huko Abidjan, Kampuni ya simu ya TECNO, ambayo ni mfadhili rasmi wa mashindano ya Kombe la Afrika ilitangaza kuwa itazindua mradi wa mpango wa hisani wa soka wa Afrika. Katika miaka mitano ijayo viwanja zaidi ya 100 vya umma vitakarabatiwa katika nchi za Afrika zaidi ya 10 zikiwemo Cote d'Ivoire, Nigeria, Senegal na Kenya.
Watu wakitazama mechi ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwa usaidizi wa mradi wa TV wa satelaiti wa China katika Kijiji cha Yaou, Cote d'Ivoire, Januari 14, 2024. (Xinhua/Han Xu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma