China na Cote d'Ivoire zaahidi kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024

ABIDJAN - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cote d'Ivoire Kacou Houadja Leon Adom siku ya Alhamisi huko Abidjan, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, huku pande zote mbili zikiahidi kuendeleza ushirikiano wa pande zote ili kupata maendeleo yenye manufaa kwa pande hizo mbili.

Adom amesema kuwa Cote d'Ivoire inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaiunga mkono China katika kutetea haki na maslahi yake halali katika Bahari ya China Kusini ambapo pia ameushukuru upande wa China kwa kujali mahitaji ya Cote d'Ivoire siku zote, na kutoa uungaji mkono mkubwa katika nyanja mbalimbali, huku akisema kuwa China imeisaidia Cote d'Ivoire kuandaa kwa mafanikio Mashindano ya 34 ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini humo.

Adom amesema, China siku zote imekuwa na udhati na urafiki kwa Afrika, ikifanya ushirikiano na Afrika kwa kuendana na kanuni ya mashauriano ya kina, mchango wa pamoja na kuchangia manufaa pamoja.

Kwa upande wake Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema China na Cote d'Ivoire ni marafiki na washirika wanaopigania maendeleo na ustawi, na kwamba ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili umepata matokeo yenye matunda mengi.

Amesema anafurahia mchango wa China katika kuandaliwa kwa mafanikio mashindano ya soka yanayoendelea, akisisitiza kuwa China ingependa kushirikiana na Cote d'Ivoire katika kuendeleza ushirikiano wa kufuata hali halisi katika nyanja mbalimbali na kuanzisha hali mpya ya uhusiano wa pande mbili katika zama mpya, chini ya mwongozo wa maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.

Amesema kuwa Cote d'Ivoire ni nchi ya mwisho katika ziara yake ya Mwaka Mpya barani Afrika, ambapo viongozi wa nchi nne za Afrika wameeleza kuunga mkono kithabiti msimamo wa serikali ya China kuhusu suala la Taiwan na kwa juhudi za China katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, hali hii imeonesha vya kutosha mila na desturi za kuungana mkono kati ya China na Afrika.

Wang pia amesisitiza kuwa, Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) limepata mafanikio makubwa katika kuongeza ushirikiano kati ya China na Afrika, hali ambayo pia imehimiza kwa nguvu jumuiya ya kimataifa kuongeza mchango barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha