China na Afrika zashirikiana kwa ajili ya maendeleo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024

Watu wanaotafuta kazi wakizungumza na waajiri kwenye maonyesho ya kazi katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Lome, mjini Lome, Togo, Novemba 24, 2023. (Picha na Yawovi Kpowoenou/Xinhua)

Watu wanaotafuta kazi wakizungumza na waajiri kwenye maonyesho ya kazi katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Lome, mjini Lome, Togo, Novemba 24, 2023. (Picha na Yawovi Kpowoenou/Xinhua)

NAIROBI - Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi katika nchi nne za Afrika inaendeleza utamaduni wa kuipa Afrika kipaumbele kwa ziara za kwanza za nje ya nchi za kila mwaka mpya unapoanza kwa mawaziri wa mambo ya nje wa China katika miaka 34 iliyopita ambapo madhumuni ya ziara hiyo ya Wang ni kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mazungumzo ya viongozi wa China na Afrika yaliyofanyika mwaka jana huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Katika mazungumzo hayo China ilitoa mapendekezo matatu ya kuunga mkono maendeleo ya viwanda, kilimo cha kisasa na kukuza watu wenye ujuzi barani Afrika, ambayo yalipokelewa vyema na Afrika.

Maendeleo ya viwanda

Wakipanda treni ya kuelekea Ibadan katika Stesheni ya Mobolaji Johnson huko Lagos, mji ambao ni kitovu cha uchumi cha Nigeria na wenye watu wengi zaidi, familia ya watu sita waliketi kwenye viti vyao katika behewa la daraja la pili, vicheko vyao vikijaza matajiro ya likizo ya Yuletide (msimu wa Krismasi).

"Nimefurahia sana safari hii," Adeniyi Salaudeen, mmoja wa wanafamilia, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano huku king’ora cha treni kikipulizwa, kuashiria kuanza kwa safari ya kuelekea Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria.

Reli hiyo iliyojengwa na China ni mfano bora wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika miundombinu. Takwimu zinaonyesha kuwa tangu Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) lianzishwe, kampuni za China zimejenga au kukarabati kilomita zaidi ya 10,000 za reli, kilomita karibu 100,000 za barabara, madaraja takribani 1,000 na bandari 100 katika nchi za Afrika. Pia zimesaidia kujenga uwezo wa kuzalisha umeme wa Kilowati milioni 120, mtandao wa mkongo wa mawasiliano wenye urefu wa kilomita 150,000 na huduma ya mtandao inafikisha watumiaji karibu milioni 700 na miradi mingine kama vile maeneo maalum ya kiuchumi na viwanda.

Nchi za Afrika zinanufaika na hatua ya China ya kuhimiza maendeleo ya viwanda, amesema Paul Frimpong, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Afrika na China cha Sera na Ushauri, taasisi ya washauri bingwa yenye makao yake makuu nchini Ghana.

Picha iliyopigwa Juni 10, 2021, ikionyesha mandhari ya nje ya Stesheni Mobolaji Johnson ya reli ya Lagos-Ibadan mjini Lagos, Nigeria. (Picha na Emma Houston/Xinhua)

Picha iliyopigwa Juni 10, 2021, ikionyesha mandhari ya nje ya Stesheni Mobolaji Johnson ya reli ya Lagos-Ibadan mjini Lagos, Nigeria. (Picha na Emma Houston/Xinhua)

Kilimo cha kisasa

Ndani ya Kituo cha Kielelezo cha Teknolojia ya Kilimo ya Msaada wa China katika Jamhuri ya Kongo, mashine zinasafisha, kumenya, kukata na kusaga kiotomatiki mihogo, chakula kikuu muhimu barani Afrika, na kugeuza mizizi ya wanga kuwa unga.

"Sasa hatuna wasiwasi tena juu ya kushindwa kukausha mihogo wakati wa mvua. Uzalishaji unafanywa kiotomatiki chini ya paa," amesema Paul Valentin Ngobo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Jamhuri ya Kongo.

Wakati huo huo, teknolojia ya Juncao, iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian nchini China, inawawezesha wakulima katika nchi nyingi za Afrika kulima uyoga kutoka kwenye nyasi kavu bila kukata miti.

Katika muongo mmoja uliopita, China imeanzisha vituo 24 vya kielelezo vya teknolojia za kilimo barani Afrika na kueneza teknolojia za hali ya juu za kilimo zaidi ya 300, ambazo zimeongeza mavuno ya mazao ya kilimo barani humo kwa wastani wa asilimia 30 hadi 60, na kunufaisha wakulima zaidi ya milioni 1 katika nchi za Afrika. Amesema Tang Renjian, Waziri wa Kilimo na Masuala ya Vijijini wa China.

Maendeleo ya watu wenye ujuzi

Uhaba wa watu wenye ujuzi, hasa katika teknolojia, unakwamisha ukuaji wa uchumi. Benki ya Maendeleo ya Afrika imekadiria nafasi mpya za ajira za kiufundi zitaongezeka milioni 4 kufikia Mwaka 2025 barani Afrika, lakini ni nusu tu zinaweza kujazwa kutokana na uhaba wa watu wenye ujuzi.

Uungaji mkono wa pande nyingi wa China kwa Afrika, ikiwa ni pamoja na miradi kama Karakana za Luban, unatoa mchango katika kujenga uwezo na uhamishaji wa maarifa katika ushirikiano kati ya China na Afrika.

Tangu kuanzishwa kwa Karakana ya kwanza ya Luban barani Afrika Mwaka 2019, China imeanzisha karakana kama hizo zaidi kumi katika bara zima, na kuvutia idadi inayoongezeka ya vijana wa Afrika wanaotafuta kuongeza ujuzi kwa ajili ya ajira na maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha