Mwanafunzi wa Sekondari ya Juu wa China afika Kilele cha Mlima Kilimanjaro na ajipanga kutembea kwa miguu kwenye miinuko ya Ncha za Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024

Xu Zhuoyuan (kushoto) akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

Xu Zhuoyuan (kushoto) akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

Siku ya Tarehe 1, Januari, 2024 Xu Zhuoyuan, mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 17 kutoka Mkoa wa Hunan, China ambaye hapo awali alishapanda kilele cha Mlima Qomolangma, alikuwa amesimama kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, kukaribisha mawio ya kwanza ya jua ya mwaka mpya.

Xu ni mchezaji mpanda milima wa ngazi ya kwanza wa China. Mwezi Mei, 2023, akiwa na umri wa miaka 16 alipanda kwenye Kilele cha Mlima Qomolangma kwa mafanikio, na kuwa mchezaji wa kike mwenye umri mdogo zaidi kufaulu kufika kilele cha mlima huo wenye urefu wa juu zaidi Duniani kwa kutokea upande wa Kusini. Tangu hapo alianzisha mpango wa "7+2", unaomaanisha kupanda vilele vya juu zaidi vya Mabara Saba Duniani, na kupanda kwa kutembea juu kwenye miinuko ya maeneo ya Ncha za Kaskazini na Kusini za Dunia.

Baada ya nusu mwaka, Xu amefika kwenye kituo cha pili cha mpango wake, Mlima Kilimanjaro, na kuupanda kwa mafanikio hadi kwenye kilele chake tarehe 1, Januari, saa 6 mchana (Kwa saa za Beijing).

Xu alianza kupanda mlima huo, kutoka upande wa Magharibi wa Mlima Kilimanjaro tarehe 27, Desemba, 2023, na alichagua njia ya Lemosho, ambayo husifiwa kwa kuwa na mandhari nzuri zaidi katika njia zote 7 za kuelekea kilele cha mlima huo. Kwa jumla alitembea kwa miguu kwa kupanda juu ya kilele kwa umbali wa kilomita 75.

“Nusu saa hadi saa moja hivi kabla ya kufika kileleni, tuliingia sehemu yenye theluji halisi. Kulikuwa na mto wa barafu mbele yake, na jua taratibu lilichomoza kutoka ukingo wa anga. Ilikuwa ni mandhari nzuri sana kwa kweli,” alisema Xu.

Kwa sasa Xu ambaye amekwisha maliza malengo mawili katika mpango wa “7+2”, anatazamiwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kumaliza mpango huo.

Xu Zhuoyuan akiwa kwenye Kilele Mlima Qomolangma tarehe 15, Mei, 2023. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

Xu Zhuoyuan akiwa kwenye Kilele Mlima Qomolangma tarehe 15, Mei, 2023. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

Xu Zhuoyuan (kulia) pamoja na mama yake Zhang Wenlin wakipanda pamoja Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa Desema, 2023. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

Xu Zhuoyuan (kulia) pamoja na mama yake Zhang Wenlin wakipanda pamoja Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa Desema, 2023. (Picha kwa hisani ya Xu Zhuoyuan/Ilichapishwa na Chinanews)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha