

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika watoa wito kwa Ethiopia, Somalia kujizuia na kupunguza mvutano
Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito kwa Ethiopia na Somalia kujizuia na kuchukua hatua za kupunguza mvutano uliopo na kuzorota kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kulikosababishwa na makubaliano ya maelewano (MoU) yaliyosainiwa kati ya nchi ya Ethiopia na eneo la Somaliland, ambalo Somalia inadai ni sehemu ya ardhi yake.
Wito huo umetolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika katika taarifa iliyotolewa kufuatia mkutano wake uliofanyika Jumatano, ulioangazia hali ya sasa ya uhusiano kati ya Ethiopia na Somalia, na kupata suluhu ya amani kwa suala hilo kwa moyo wa masuluhisho ya Kiafrika kwa matatizo ya Kiafrika.
Umoja wa Afrika umezihimiza nchi hizo mbili kujiepusha na vitendo na kauli zaidi zinazoweza kuathiri vibaya ukaribu uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Baraza hilo pia limeonesha "wasiwasi wake mkubwa" kuhusu mvutano unaoendelea kati ya nchi hizo mbili na athari zinazoweza kutokea kwa amani, usalama na utulivu wa kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma