

Lugha Nyingine
Nchi zisizofungamana na upande wowote zashinikiza kuwa na sauti zaidi katika masuala ya kimataifa
Nchi wanachama wa Harakati ya Nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) zinazoendelea na mkutano nchini Uganda, zimeshikilia msimamo wa kuhakikisha kuwa harakati hiyo yenye nchi wanachama 120 ina sauti zaidi katika masuala ya kimataifa.
Makamu wa Rais wa Uganda Bibi Jessica Alupo, amesema wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa harakati hiyo, kuwa Harakati hiyo inafanya mkutano wake wakati ambapo mivutano ya siasa za kijiografia inaongezeka.
Amesema kutokana na kuwepo kwa matukio kama haya kwenye mikutano ya kimataifa, nchi wanachama zinapaswa kuwa na umoja na kushikamana na kufuata kanuni za msingi za Harakati hiyo, ikiwa ni pamoja na kuheshimu uhuru na ukamilifu wa ardhi za mataifa yote, kutambua usawa wa rangi zote na usawa wa mataifa yote, makubwa na madogo, na kujiepusha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma