

Lugha Nyingine
Rais wa Cote d'Ivoire asisitiza tena nchi yake kufuata sera ya kuwepo kwa China moja
Rais Alassane Ouattara wa Cote d'lvoire Jumatano alikutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi mjini Abidjan, na kusisitiza msimamo wa nchi yake wa kufuata sera ya kuwepo kwa China moja.
Bwana Ouattara amemwomba Bw. Wang kufikisha salamu zake kwa Rais Xi Jinping, na kumpongeza Rais Xi kwa falsafa ya utawala inayojali maslahi ya watu.
Amesema anafurahia mafanikio makubwa ya China, na ameishukuru China kwa kubeba majukumu kama nchi inayohimiza amani na maendeleo.
Wakati huo huo Bwana Wang alikutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Cote d’Ivoire Bw. Kacou Houdja Leon Adom, mawaziri hao wameahidi kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana wa pande zote. Bwana Adom pia amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma