

Lugha Nyingine
Serikali ya Rwanda yapanga kuziondoa familia zaidi ya laki 3 kutoka kwenye umaskini katika miaka miwili
Serikali ya Rwanda imepanga kuziondoa kaya 315,000 kutoka kwa umaskini na umaskini uliokithiri katika kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa ulioidhinishwa na Baraza la Mawaziri la Rwanda Novemba 2022 ili kuongeza kasi ya kupunguza umaskini na umaskini uliokithiri nchini Rwanda.
Mkakati huo unalenga kusaidia kaya zote zilizo katika umaskini uliokithiri kuwa na maisha endelevu yanayohimili mishtuko ya wastani, na hatimaye kuziondoa kabisa katika umaskini.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Taasisi za Tawala za Mitaa (LODA), Bibi Claudine Nyinawagaga amesema kwa ujumla, wanahitaji kuzikwamua kaya laki 9 kutoka kwenye mazingira magumu, lakini kwa mwaka huu wanaanza na kaya laki 3.15.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma