Sudan yasitisha uanachama wake IGAD

(CRI Online) Januari 22, 2024

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan Jumamosi imetangaza kuwa, nchi hiyo imesitisha uanachama wake katika Shirika la Kiserikali kwa Maendeleo la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

Taarifa ya Wizara hiyo imesema, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan amemwarifu mwenyekiti wa IGAD wa sasa juu ya uamuzi wa Sudan wa kusitisha uanachama wake katika Shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo ya Sudan imekuja baada ya IGAD kupuuza uamuzi wa Sudan uliowasilishwa kwenye Shirika hilo, wa kutozungumzia masuala yoyote yanayohusiana na Sudan, jambo ambalo halikutokea katika mkutano maalum wa IGAD uliofanyika nchini Uganda Alhamis wiki iliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha