Video: Meli ya Fu yasafiri kutoka Quanzhou, China kwenda duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2024

Meli ya Fu ni jina jumuishi kwa meli za mbao za kusafiri baharini zinazoundwa kwenye maeneo ya pwani ya Mkoa wa Fujian, China. Meli ya aina hiyo yenye umbo la kina kirefu na upana katika sehemu ya juu inafaa kusafiri baharini.

Ikiwa ni sehemu ya kuanzia ya Njia ya Hariri ya Baharini katika wakati wa Enzi ya Song (B.K. 960-1279) na Enzi ya Yuan (B.K. 1271-1368), Mji wa Quanzhou ulikuwa na ustawi wa shughuli za biashara kwenye bahari na kazi za uundaji wa meli, hivyo mji huo ulikuwa kituo cha uundaji wa meli cha nchi nzima.

Katika wakati huo, meli za wafanyabiashara zilizosafiri kwa kupitia njia ya hariri ya bahari kwenda Asia ya Kaskazini Mashariki, Asia ya Kusini Mashariki, Bahari ya Hindi, nchi za Kiarabu na pwani ya Afrika ya Mashariki, nyingi kati yao ni meli za Fu.

“Msingi muhimu zaidi wa ubebaji wa meli ya Fu ni mgongo wake wa chini ya meli, ambao unatengenezwa kwa nyenzo nzito zenye unene wa kiwango cha juu. Ni sehemu nzito zaidi ya meli nzima. Inaweza kuifanya meli ya Fu kuwa kama bilauri na kuhimili upepo mkali na mawimbi makubwa,” amesema Lin Peizong, mrithi wa kizazi cha 11 wa ufundi wa kutenganisha sehemu za meli.

Ufundi wa kutenganisha sehemu za meli ni moja kati ya teknolojia muhimu zaidi za ujenzi wa meli ya Fu. Sehemu zinagawanywa katika sehemu maalumu mbalimbali kwa kutumia kibao cha kutenga, ili kuimarisha meli na kuzuia na kutenga maji.

“Mpaka hivi leo, meli za kisasa za China kama vile nyambizi, manowari ya kubeba ndege za kivita n.k. bado zinatumia ufundi wa kutenganisha sehemu za meli,” amesema Lin.

Mnamo mwaka 2010, “Ufundi wa China wa uundaji meli ya Fu kwa kutenganisha sehemu mbalimbali za meli” uliorodheshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwenye “orodha ya urithi wa mali ya utamaduni usioshikika unaohitaji kuhifadhiwa kwa dharura”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha