China yatoa wito wa juhudi zaidi katika kuendeleza ushirikiano wa Kusini na Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2024

KAMPALA - Mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China Liu Guozhong alihudhuria Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi za Kusini uliofanyika Jumapili katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, ambapo alitoa hotuba akitoa wito wa kuhimiza ushirikiano wa Kusini na Kusini na mageuzi ya mfumo wa utawala wa kimataifa.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Kundi la nchi 77, na katika kipindi cha miongo sita iliyopita, nchi za Kusini zimefuata njia sahihi ya usawa, kuaminiana, kunufaishana, kushikamana na kusaidiana, amesema Liu, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Naibu Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China.

Uhuru ndiyo sifa maalum ya kisiasa ya nchi za Kusini, kujiendeleza kupitia mshikamano ni desturi ya nchi za Kusini, maendeleo na ustawishaji ni dhamira ya kihistoria ya nchi za Kusini, na haki na usawa ni mapendekezo ya pamoja ya nchi za Kusini, Liu amebainisha.

Mageuzi ya Dunia ambayo hayajaonekana katika miaka 100 iliyopita yanajitokeza kwa kasi kubwa, na nchi za Kusini zinakabiliwa na mazingira magumu ya nje, amesema, huku akitoa wito kwa juhudi zaidi katika kutafuta njia ya maendeleo ya kisasa, kuhimiza ushirikiano wa Kusini na Kusini katika kiwango cha juu, kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya mfumo wa utawala wa kimataifa, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ambayo ni unganishi, yenye usawa, uwiano na manufaa kwa wote.

Liu amesema kuwa Rais wa China ametoa maono muhimu ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, pamoja na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, ukilenga kuhamasisha rasilimali za kimataifa, kuhimiza maendeleo ya pamoja ya jamii ya binadamu, utulivu wa muda mrefu na kufunzana kati ya ustaarabu mbalimbali, na kusukuma Dunia kuelekea mustakabali mzuri wa amani, usalama, ustawi na maendeleo.

Mkutano wa wakuu wa nchi za Kusini ndiyo chombo kikuu cha kufanya maamuzi cha Kundi la nchi 77. Wawakilishi wa ngazi ya juu wa nchi karibu 100 na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa walihudhuria mkutano huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha