

Lugha Nyingine
Mkutano wa kilele wa 19 wa harakati ya nchi zisizofungamana na upande wowote wafungwa mjini Kampala
Mkutano wa kilele wa 19 wa harakati ya jumuiya ya nchi zisizofungamana na siaza za upande wowote (NAM) ulifungwa tarehe 20 Januari mjini Kampala, Uganda huku “Azimio la Kampala” lililopitishwa likitoa wito wa kushikilia ushirikiano wa pande nyingi, kuimarisha ushawishi wa NAM kwenye mambo ya kimataifa, na kuweka jitihada katika kujenga dunia yenye amani, haki na ustawi.
“Azimio la Kampala” linasisitiza tena kanuni zilizowekwa mwaka 1961 kwenye mkutano wa Bandung wa mwaka 1955 na kuanzishwa kwa harakati hiyo, na kusisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini na Kusini na Kaskazini, kuheshimu kwa pande zote sheria za kimataifa na kanuni za makubaliano ya kimataifa, kukabiliana kwa pamoja na matishio na changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Azimio la Kampala” pia limelaani vikali operesheni ya kijeshi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, na kutoa wito usimamishaji mara moja wa vita wa kibinadamu na wa kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma