Umeme wa Kilowati 100 waanza kuingizwa kwenye gridi ya taifa nchini Tanzania

(CRI Online) Januari 23, 2024

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati wa Tanzania Dk Doto Biteko, amesema majaribio ya mtambo namba tisa kwenye mradi wa kuzalisha umeme kwa maji wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) yamekuwa na mafanikio makubwa na umeme wa kilowati 100 umeanza kuingizwa kwenye gridi ya taifa.

Dk Biteko ameeleza kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na wakandarasi na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akisema amefurahishwa na taarifa iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Kampuni ya Elsewedy, Mhandisi Wael Hamdy kuhusu majaribio hayo.

Kwa mujibu wa habari zilizoelezwa, maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Arab Contractors ya Misri kwa sasa yamefikia asilimia 95.83.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha