

Lugha Nyingine
China yasema iko tayari kushirikiana na washirika wa kimataifa kuunga mkono Nchi ya Visiwa vya Comoro kudumisha utulivu wa kijamii
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China iko tayari kushirikiana na washirika wa kimataifa kuunga mkono Nchi ya Visiwa vya Comoro kudumisha utuliuvu wa kijamii, ili kuchangia katika maendeleo ya amani ya nchi hiyo.
Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Wang Wenbin amesema, tangu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Comoros ilipotangaza kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo Azali Assoumani ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu tarehe 16 Januari, wafuasi wa upinzani wamekuwa wakiandamana katika sehemu mbalimbali nchini humo, huku Marekani, Umoja wa Ulaya na Ufaransa zikitoa taarifa kuonesha mashaka juu ya matokeo ya uchaguzi huo.
Bw. Wang amesisitiza kuwa, uchaguzi wa rais ni mambo ya ndani ya Visiwa vya Comoro, na kwamba China siku zote inashikilia kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kuhehsimu matakwa na chaguo la wananchi wa Visiwa vya Comoro.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma