Mwakilishi maalumu wa Rais wa China ashiriki kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Liberia

(CRI Online) Januari 23, 2024

Mwakilishi maalumu wa Rais wa China Bw. Bate'er ameshiriki kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais Joseph Nyumah Boakai wa Liberia iliyofanyika Jumatatu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Monrovia.

Kabla ya hapo, Rais mteule Boakai alikutana na Bw. Bate’er siku ya Jumapili, ambapo Bw. Bate’er alimpa salamu kutoka kwa Rais Xi Jinping, na kusema China inatilia maanani uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na iko tayari kushirikiana na Liberia kuzidisha maelewano, kuimarisha ushirikiano na kuhimiza uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha