Spika wa Bunge la Umma la China afanya mazungumzo na spika wa Bunge la Djibouti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2024

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Dileita Mohamed Dileita, Spika wa Bunge la Djibouti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 23, 2024. (Xinhua/ Zhai Jianlan)

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Dileita Mohamed Dileita, Spika wa Bunge la Djibouti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China amefanya mazungumzo na Dileita Mohamed Dileita, Spika wa Bunge la Djibouti siku ya Jumanne mjini Beijing ambapo amesema chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, China na Djibouti zimezidisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuendeleza kwa kasi ushirikiano wenye matokeo halisi na kufanya mawasiliano yenye manufaa kati ya watu.

Amesema China ingependa kushirikiana na Djibouti katika kusukuma mbele ushirikiano wao wa kimkakati, na daima imekuwa ikitendea na kuendeleza uhusiano wake na Djibouti kwa muono wa muda mrefu na wa kimkakati.

“China inaishukuru Djibouti kwa uungaji wake mkono muhimu katika masuala yanayohusu Taiwan, Xinjiang, Hong Kong na haki za binadamu” Zhao amesema huku akiongeza kuwa China itaendelea kuiunga mkono Djibouti katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na utulivu wake, katika kutafuta kwa kujiamulia njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika masuala ya kimataifa na kikanda.

Amesema China ingependa kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo ya Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na kupanua ushirikiano katika bandari, maeneo maalum ya biashara huria, uwekezaji na ujenzi wa miundombinu.

Ameeleza kuwa China inathamini uungaji mkono wa Djibouti kwa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kupenda kutoa mchango mpya katika ujenzi wa jumuiya ya kiwango cha juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake Dileita amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Djibouti na China miaka 45 iliyopita, ushirikiano wa pande mbili katika siasa, uchumi, utamaduni na maisha ya watu umekuwa na matokeo mazuri.

Amesema Djibouti siku zote inafuata kwa uthabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na Bunge la Djibouti ingependa kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na Bunge la Umma la China. 

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Dileita Mohamed Dileita, Spika wa Bunge la Djibouti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 23, 2024. (Xinhua/ Zhai Jianlan)

Zhao Leji, Spika wa Bunge la Umma la China, akifanya mazungumzo na Dileita Mohamed Dileita, Spika wa Bunge la Djibouti, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 23, 2024. (Xinhua/ Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha