Juhudi za pande zote za kutafuta manusura wa maporomoko ya ardhi zaendelea huku idadi ya vifo ikiongezeka hadi 31 Kusini Magharibi mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2024

KUNMING - Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyokumba kijiji cha milimani katika Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China siku ya Jumatatu imeongezeka na kufikia watu 31 hadi saa 11:40 jioni kwa saa za Beiijing siku ya Jumanne, mamlaka za serikali za mitaa zimesema ambapo waokoaji zaidi ya 1,000 wamejiunga katika shughuli za uokoaji, ikiwa ni pamoja na mashine za uchimbuaji na magari 150 na mbwa 81.

Waokoaji wakifanya shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Waokoaji wakifanya shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Miongoni mwa watu 47 walioripotiwa kutojulikana walipo hapo awali, waokoaji wamefanikiwa kuwasiliana na watatu, ambao hawakuwa karibu na maporomoko hayo ya ardhi lakini hawakuweza kufikiwa kwa mawasiliano, kwa mujibu wa makao makuu ya utoaji msaada wa maafa ya eneo hilo.

Wakazi jumla ya 918 kutoka familia 223 wamehamishwa hadi maeneo salama. Baadhi wanakaa na jamaa, na wengine wanakaa katika makazi ya muda katika shule iliyo karibu. Wakazi wawili wanapokea matibabu hospitalini.

Maafa ya ghafla

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea majira ya saa 12 ausbuhi ya siku ya Jumatatu kwa saa za Beijing katika Kijiji cha Liangshui, Wilaya ya Zhenxiong, katika mji wa Zhaotong.

Mwanakijiji Hong Xianjie aliamshwa na sauti ya kishindo iliyoambatana na maporomoko hayo.

"Nilihisi ardhi ikitetemeka. Nilidhani ni tetemeko la ardhi," amekumbuka Hong, ambaye alipata bahati ya kutoka bila kujeruhiwa kwenye janga hilo.

Waokoaji wakifanya shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Waokoaji wakifanya shughuli za uokoaji katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Mahema zaidi ya 200, makoti 1,200 ya pamba, mablanketi 700, vitanda 200 vya kukunjwa na vifaa vingine vimepelekwa kwenye eneo la maafa.

Kukimbizana na wakati

Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa maporomoko hayo ya ardhi yamesababishwa na kuporomoka katika eneo lenye miinuko mikali ya miamba juu ya mteremko. Mvua za awali pia zimesababisha maporomoko hayo.

Waokoaji wanakimbizana na wakati kutafuta watu wasiojulikana waliko, lakini hali ya hewa ya baridi na theluji inatatiza juhudi zao.

Waokoaji wakiweka vifaa vya radi katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Waokoaji wakiweka vifaa vya radi katika Kijiji cha Liangshui kilichoko Tarafa la Tangfang, Mji wa Zhaotong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Januari 23, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

"Tunatumia mashine za kuchimbua kusafisha njia kabla ya kuondoa mawe kwa mikono ili kupata watu waliozikwa," amesema Chen Pinrun, mfanyakazi wa zimamoto. "Wakati ni maisha. Tutafanya kila tuwezavyo kuokoa maisha."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha