

Lugha Nyingine
China yasema iko tayari kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ugaidi na nchi nyingine
Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka kuhusu "Mfumo na Utekelezaji wa Sheria ya Kupambana dhidi ya Ugaidi wa China" siku ya Jumanne.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Wang Wenbin amesema, China iko tayari kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine katika mapambano dhidi ya ugaidi, kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mapambano dhidi ya ugaidi duniani, kuhimiza maendeleo mazuri ya mapambano hayo, na kudumisha amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.
Bw. Wang amesema, waraka huo unaeleza kwa kina na kwa utaratibu mfumo na utekelezaji wa sheria ya mapambano ya China dhidi ya ugaidi, ikiwa ni pamoja na viwango vya utambuzi na kanuni za adhabu kwa vitendo haramu na uhalifu wa vitendo vya kigaidi, na kanuni za utekelezaji wa mamlaka katika kazi ya mapambano na kulinda haki za binadamu kwa kufuata sheria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma