Rais wa Tanzania aliagiza jeshi kuwa macho kuhakikisha uchaguzi ujao unafanyika kwa amani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 24, 2024

Picha hii iliyopigwa Desemba 29, 2023 ikionyesha bandari ya Dar es Salaam wakati wa machweo mjini Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Wang Guansen)

Picha hii iliyopigwa Desemba 29, 2023 ikionyesha bandari ya Dar es Salaam wakati wa machweo mjini Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Wang Guansen)

DAR ES SALAAM - Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mji wa kibiashara wa Dar es Salaam, Tanzania ameliagiza jeshi hilo kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unafanyika katika hali ya amani na kwamba jeshi linapaswa kujiandaa kwa changamoto zozote zinazoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi.

Tanzania itafanya uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu kuchagua viongozi katika ngazi ya chini, na uchaguzi mkuu Oktoba 2025 wa kuchagua rais, wabunge na madiwani.

Rais Samia, ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya Tanzania, amesema kwa kuwa uchaguzi unahusiana na vyama vingi vya siasa vilivyo na nia tofauti, ni jambo la busara kwa wanajeshi kukaa macho.

Hata hivyo, Rais Samia ameeleza kuwa maneno aliyosema hayamaanishi kwamba machafuko kweli yatatokea katika uchaguzi, huku akiongeza kuwa, hitaji la lazima la kuimarisha usalama linakuwa muhimu zaidi katika wakati wa uchaguzi.

Picha hii iliyopigwa Septemba 22, 2023 ikionyesha  mwonekano wa Mji wa Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa Septemba 22, 2023 ikionyesha mwonekano wa Mji wa Dar es Salaam, Tanzania. (Xinhua/Dong Jianghui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha