Lugha Nyingine
Wafanyabiashara wa China kujenga mabweni na visima Dar es salaam, Tanzania
(CRI Online) Januari 24, 2024
Katika hali ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa mabweni kwa wanafunzi hususan wanafunzi wa kike nchini Tanzania, Chama cha Wafanyabiashara wa Jiangsu nchini Tanzania, kimejitolea kujenga mabweni mawili na kuchimba visima vitano vya maji safi na salama.
Ahadi hiyo imetolewa na mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Tony Zhang alipotoa salamu za umoja huo kwenye sherehe za mwaka mpya zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobras Katambi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ACTL), Ladislaus Matindi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Jumanne Muliro.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



