Nchi zinazotumia Ziwa Victoria zakutana kujadili uchafuzi katika Ziwa hilo

(CRI Online) Januari 24, 2024

Wawakilishi kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi wamekutana jijini Dar es Salaam, Tanzania, kwa lengo la kujadili uchafuzi unaosababishwa na vitendo vya binadamu katika Ziwa Victoria.

Msimamizi wa mradi wa maendeleo katika Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Hilda Luoga amesema katika mkutano huo kuwa, mradi wenye thamani ya dola bilioni 2 za kimarekani unaolenga kurejesha hadhi ya Ziwa Victoria unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Amesema mradi huo utakaotekelezwa chini ya Kamisheni hiyo kwa miaka kumi, unahusisha kudhibiti taka ngumu, usafi na mifumo ya majitaka inayochafua Ziwa Victoria, na kuonya kuwa, Ziwa hilo linalotumiwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, linakabiliwa na uchafuzi mkubwa unaotokana na vitendo vya binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha