Lugha Nyingine
China na Nauru zarejesha uhusiano wa kidiplomasia
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea, na kutia saini taarifa ya pamoja ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia wa pande mbili katika ngazi ya kibalozi mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
BEIJING - China na Nauru zimetia saini taarifa ya pamoja mjini Beijing Jumatano kuhusu kurejesha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya kibalozi ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea na kutia saini taarifa hiyo ya pamoja, ambayo yameanza kutekelezwa mara moja kuanzia siku hiyo.
Taarifa hii imeifanya Nauru kuwa nchi ya 183 kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na China.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya pamoja, Serikali ya Jamhuri ya Nauru inatambua kuwa kuna China moja tu duniani, Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo Serikali pekee halali inayowakilisha China nzima, na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya China.
Taarifa hiyo ya pamoja imesema kwamba Serikali ya Jamhuri ya Nauru itavunja "uhusiano ya kidiplomasia" na Taiwan kuanzia leo (jana Jumatano) na kuahidi kwamba haitaanzisha tena uhusiano wowote rasmi au mawasiliano rasmi na Taiwan.
Serikali hizo mbili zimekubaliana kuteua mabalozi mapema iwezekanavyo na kupeana msaada unaohitajika kwa ajili ya kuanzisha balozi, imesema taarifa hiyo ya pamoja.
"Leo, uhusiano kati ya China na Nauru umefungua ukurasa mpya," Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kwenye mazungumzo hayo.
Wang amesema ingawa China na Nauru zinatenganishwa kijiografia na bahari, urafiki kati ya watu wa pande hizo mbili una historia ndefu. Zikiwa ni nchi zinazoendelea, pande zote mbili zinakabiliwa na majukumu ya pamoja ya kuendeleza uchumi, kuboresha maisha ya watu na kufikia maendeleo ya kisasa.
Wang amedokeza kuwa bado kuna nchi chache sana zinazodumisha kile kinachoitwa "uhusiano wa kidiplomasia" na Taiwan kwa sababu mbalimbali, ambazo siyo tu zinakwenda kinyume na maslahi ya nchi zao na watu wao, lakini pia zinakiuka azimio Namba 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kukiuka mamlaka ya kitaifa ya China. Vitendo kama hivyo vinapaswa kusahihishwa mapema au baadaye.
China inazitaka nchi hizo kutambua mwelekeo wa nyakati, amesema Wang na kuongeza kuwa China inapenda kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wake na nchi hizo juu ya msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea, na kutia saini taarifa ya pamoja ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia wa pande mbili katika ngazi ya kibalozi mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea, na kutia saini taarifa ya pamoja ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia wa pande mbili katika ngazi ya kibalozi mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Shen Hong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma