Waziri Mkuu wa China Li Qiang afanya mazungumzo na mwenzake wa Antigua na Barbuda Gaston Browne

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya hafla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gaston Browne katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Yin Bogu )

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya hafla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gaston Browne katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya mazungumzo na mwenzake wa Antigua na Barbuda Gaston Browne mjini Beijing siku ya Jumatano akisema kwamba tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 41 iliyopita, China na Antigua na Barbuda zimekuwa zikiheshimiana na kuungana mkono na kwamba China inapenda kushirikiana na Antigua na Barbuda kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.

Akibainisha kuwa nchi zote mbili ni nchi zinazoendelea, Waziri Mkuu Li amesema China itashirikiana na Antigua na Barbuda kuendeleza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuimarisha ushirikiano katika kilimo na miundombinu, na kujikita zaidi katika uwezekano wa ushirikiano katika sekta ya uchumi wa kijani, uchumi wa baharini na kidijitali ili kuendeleza nguvu mpya za maendeleo ya kiuchumi.

Waziri Mkuu Li amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya watu na ya kitamaduni katika nyanja za utalii, usafiri wa anga, tiba na afya na rasilimali watu. Amebainisha kuwa China, inapenda kutoa uungaji mkono iwezavyo kwa Antigua na Barbuda katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi chini ya mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kuendelea kuimarisha uratibu na ushirikiano wa pande nyingi ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake Browne amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Antigua na Barbuda na China, uhusiano wa pande mbili umedumisha kasi kubwa ya maendeleo. Ameelezea shukrani zake kwa uungaji mkono mkubwa wa China kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Antigua na Barbuda kwa miaka mingi, na uungaji mkono wake kwa mapendekezo muhimu ya China kama vile Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia moja.

Amesema Antigua na Barbuda inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaamini kwamba Taiwan ni mkoa wa China, na inaiunga mkono kwa dhati China katika kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi yake.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gaston Browne kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Gaston Browne kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha