

Lugha Nyingine
Mahakama Kuu ya Comoro yamtangaza Azali Assoumani kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo
(CRI Online) Januari 25, 2024
Mahakama Kuu ya Comoro jana Jumatano ilitangaza kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo Azali Assoumani amechaguliwa tena kuendelea na madaraka yake baada ya kupata zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa katika upigaji kura wa duru ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Comoro, mgombea anayepata kura zaidi ya nusu katika duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu anatangazwa kuwa mshindi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma