

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa UN atoa wito wa kuchukua hatua za haraka kupambana dhidi ya ugaidi barani Afrika
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza haja ya kukabiliana na ongezeko la ugaidi barani Afrika, akiielezea hali hiyo kuwa ni hatari ya wazi siyo tu kwa bara hilo, bali kwa dunia nzima.
Akizungumza katika mkutano wa Mkataba wa Kupambana dhidi ya Ugaidi Duniani uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, Guterres amesema katika miaka michache, Afrika imekuwa kituo cha ugaidi duniani, na kwamba katika mazingira hayo, wanawake na watoto wa kike wako hatarini zaidi kufanyiwa unyanyasaji wa kimapenzi na uhalifu wa kijinsia.
Amesema katika maeneo kama Somalia, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kaskazini mwa Msumbiji na kanda ya Sahel, raia wanakabiliwa na mapigano na machafuko, wakiishi maisha magumu yasiyo na matumaini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma