

Lugha Nyingine
Nchi wanachama wa NAM zaipongeza China kwa juhudi zake za kudumisha amani ya dunia
Maofisa wa ngazi ya juu kutoka Uganda, Sudan na Bolivia wameipongeza China kwa mchango wake katika kuboresha usawa katika masuala ya kimataifa.
Wakizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua wakati wa mkutano wa 19 wa Harakati za Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siaza za Upande Wowote (NAM) uliofanyika nchini Uganda, maofisa hao wamesema China imekuwa ikichukua nafasi muhimu katika ustawi wa kisiasa, kijamii na kiuchumi katika nchi zinazoendelea.
Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Al-Sadiq amesema, China ni mshirika muhimu wa Afrika, kwa kuwa nchi hiyo imejikita katika maendeleo ya nchi za Afrika bila ya kuwa na masharti yoyote.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Okello Oryem amepongeza mchango wa China katika kutatua mgogoro unaoendelea katika Ukanda wa Gaza, na kusema China daima imekuwa mtetezi wa suluhu ya amani katika migogoro.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Bolivia, Celinda Sosa Lunda ameielezea China kama mshirika wa maendeleo wa nchi hiyo, na kusema Bolivia inaungana na msimamo wa China katika kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma