Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wa Kenya, Musalia Mudavadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Musalia Mudavadi mjini Beijing, China, Januari 25 , 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Musalia Mudavadi mjini Beijing siku ya Alhamisi ambapo amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 60 iliyopita, China na Kenya siku zote zimekuwa na maelewano na kuungana mkono, na kwamba zimekuwa marafiki wazuri wanaoaminiana na washirika wazuri wa kunufaishana.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amesema, wakuu wa nchi hizo mbili wameanzisha uaminifu na urafiki, wakitoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

China inapongeza Kenya kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kuiunga mkono Kenya kwa uthabiti katika kulinda mamlaka, uhuru na utulivu wa taifa, na kuhimiza maendeleo yake kwa kujitegemea, Wang amesema, huku akiongeza kuwa China inapenda kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na Kenya, kuimarisha ushirikiano wa pande zote, na kuinua uhusiano kati ya China na Kenya kwenye ngazi mpya.

Mudavadi amesema kuwa ushirikiano wa kivitendo kati ya Kenya na China umepata matokeo makubwa, na kwamba ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umetoa uungaji mkono mkubwa kwa ujenzi wa taifa la Kenya na maendeleo yake ya kiuchumi.

Kwa niaba ya serikali ya Kenya, Mudavadi amesisitiza tena kuwa Kenya itaendelea kufuata bila kuyumba kanuni ya kuwepo kwa China moja na kusimama na China katika masuala kama vile Taiwan na haki za binadamu, na kusema kuwa Kenya inatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano kati yake na China.

Kenya inathamini sana ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa wote, pamoja na mfululizo wa mapendekezo muhimu ya kimataifa yanayotolewa na China, na inapenda kuendelea kushiriki kikamilifu kwenye mapendekezo hayo, amesema, huku akiongeza kuwa Kenya inatarajia kujifunza kutoka kwa dhana za maendeleo za China na kuimarisha mawasiliano ya uzoefu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Musalia Mudavadi mjini Beijing, China, Januari 25 , 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya Musalia Mudavadi mjini Beijing, China, Januari 25 , 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha