

Lugha Nyingine
China yapenda kutumia kikamilifu fursa za ushirikiano na Japan: Waziri Mkuu
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na ujumbe wa wafanyabiashara wa Japan unaoongozwa na Mwenyekiti wa Shirika la Biashara la Japan Masakazu Tokura, Mwenyekiti wa Shirikisho la Uchumi la Japan na China Kosei Shindo, na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara na Viwanda la Japan Ken Kobayashi kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Januari 25, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
BEIJING - China itaunga mkono kampuni za China na Japan kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na inakaribisha kampuni kutoka nchi zote ikiwa ni pamoja na Japan kuendelea kuwekeza nchini China, Waziri Mkuu Li Qiang amesema siku ya Alhamisi alipokutana na ujumbe wa wafanyabiashara wa Japan unaoongozwa na Mwenyekiti wa Shirika la Biashara la Japan, Masakazu Tokura, Mwenyekiti wa Shirikisho la Uchumi la Japan na China, Kosei Shindo, na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyabiashara na Viwanda la Japan, Ken Kobayashi.
Huku akieleza kuwa uhusiano kati ya China na Japan uko katika hatua muhimu ya kuendeleza urithi wa zamani na kufungua mustakabali wa baadaye, Waziri Mkuu Li amewataka wadau wa biashara wa nchi hizo mbili kuendelea kujitoa kwa mwelekeo sahihi wa amani, urafiki na ushirikiano na kuurudisha uhusiano kati ya China na Japan kwenye njia ya maendeleo mazuri.
"Uchumi wa China na Japan umeunganishwa kwa kina, na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara unatoa mchango mkubwa kama msingi na kichocheo cha uhusiano wa pande mbili," Waziri Mkuu Li amesema, na kuongeza kuwa China inapenda kuendelea kunufaisha fursa za maendeleo, kuunga mkono kampuni za nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, huduma za tiba na utunzaji wa wazee, kuhakikisha kwa pamoja uendeshaji thabiti na mzuri wa minyororo ya viwanda na usambazaji, na kufikia kuendana kwa kiwango cha juu na matokeo yenye manufaa kwa pande zote.
Ameelezea matumaini yake kuwa Japan itatoa mazingira ya biashara ya wazi, ya haki na yasiyo na ubaguzi kwa kampuni za China nchini Japan.
Wakuu wa makundi hayo matatu ya kibiashara yaliyotajwa hapo juu kutoka Japan wameonyesha matumaini kwamba nchi hizo mbili zitarejea kwenye matarajio ya awali ya urafiki, na kuimarisha mawasiliano katika sekta zote na katika ngazi zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma