China yakabidhi vifaa vya kusaidia kuijengea uwezo Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2024

Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui (Kulia) na Etambuyu Gundersen, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia, wakishiriki hafla ya makabidhiano mjini Lusaka, Zambia, Januari 25, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui (Kulia) na Etambuyu Gundersen, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia, wakishiriki hafla ya makabidhiano mjini Lusaka, Zambia, Januari 25, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

LUSAKA - China imekabidhi vifaa vya kusaidia ujenzi wa uwezo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia siku ya Alhamisi ambapo vifaa hivyo vinavyojumuisha kompyuta mpatao 20 na printa 20 vimekabidhiwa na Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui katika hafla iliyohudhuriwa na Etambuyu Gundersen, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, na maafisa wengine kutoka wizara hiyo na ubalozi wa China.

"Hii ni hatua ya kwanza tu. Tunakusanya rasilimali zaidi kusaidia wizara yako," balozi wa China amesema.

Amesema China pia inatoa programu zaidi za mafunzo kwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, hasa kwa wanadiplomasia vijana, huku akiongeza kuwa anatumai kuwa vifaa na programu hizo za mafunzo zitageuka kuwa matokeo ya mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili yenye hali ya kuaminiana na ufanisi wa hali ya juu.

Aidha ameeleza kuwa China itaendelea kuwa fursa ya maendeleo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Zambia na kuongeza kuwa China inapenda kushirikiana na sekta zote nchini Zambia ili kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili kwenye mkutano wa mwaka jana.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara wa Zambia ameishukuru China kwa msaada huo, akisema utasaidia kujenga uwezo wa wanadiplomasia vijana katika kujenga uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia na nchi nyingine ikiwemo China.

Amesema, msaada huo siyo tu unawakilisha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, lakini pia moyo wa urafiki ambao China imeonyesha katika miaka 60 iliyopita.

Amesema uhusiano wa kirafiki umeonyeshwa katika nyanja kama vile miundombinu, elimu, na mawasiliano ya kiutamaduni. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha