

Lugha Nyingine
Bendera ya Taifa la China yapandishwa Nauru baada ya miaka 19 iliyopita
Ujumbe wa wanadiplomasia wa China wenye wajibu wa kujenga upya ubalozi wa China nchini Nauru ukifanya hafla ya kupandisha bendera ya Taifa la China katika Jamhuri ya Nauru, Januari 29, 2024. (Picha na Chen Guolong/Xinhua)
YAREN – Hafla ya kupandisha bendera ya Taifa la China imefanyika leo Jumatatu nchini Nauru na ujumbe wa wanadiplomasia wa China, hii ni mara ya kwanza kwa bendera hiyo nyekundu ya nyota tano kupandishwa katika nchi hiyo ya kisiwa cha Pasifiki baada ya miaka 19 iliyopita.
Hafla hiyo imefanywa na ujumbe wenye wajibu wa kujenga upya ubalozi wa China nchini Nauru katika eneo la ua kubwa ambalo hivi sasa lina ofisi za muda za ujumbe huo.
Wang Xuguang, kiongozi wa ujumbe wa wanadiplomasia hao, amewaambia waandishi wa habari kwamba China na Nauru kiasili zinasaidiana na zina uwezo mkubwa wa kifursa katika ushirikiano wa pande mbili.
"Nina uhakika zaidi juu ya ushirikiano wa siku zijazo kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali," Wang amesema.
“Kwa kuendelea mbele, pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha kuendana kwa mikakati yao ya maendeleo, kujitahidi kutafuta maeneo ya pamoja ya ushirikiano, na kutekeleza miradi mingi na bora zaidi ili watu wa nchi hizo mbili waweze kunufaika na uhusiano wa pande mbili kwa mapema zaidi,” amesema.
Serikali ya Nauru ilitoa taarifa Januari 15, na kutangaza kwamba inatambua kanuni ya kuwepo kwa China moja, ikavunja kile kinachoitwa "uhusiano wa kidiplomasia" na eneo la Taiwan, na kwamba ingependa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati yake na China.
China na Nauru zilitia saini taarifa ya pamoja mjini Beijing Januari 24 kuhusu kurudishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia wa ngazi ya kibalozi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma