ECOWAS yathibitisha Burkina Faso, Mali, Niger kuwa wanachama licha ya madai ya kujitoa kwa wanajeshi waliopindua serikali

(CRI Online) Januari 29, 2024

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) yenye nchi wanachama 15, imesisitiza kuwa Burkina Faso, Mali, na Niger bado ni nchi wanachama wa jumuiya hiyo, wakijibu tamko la awali la mamlaka za kijeshi katika nchi hizo, kueleza nia ya kujiondoa uanachama kwenye jumuiya hiyo.

ECOWAS imesema katika taarifa yake kuwa haijapokea taarifa yoyote ya moja kwa moja kutoka kwa nchi hizo tatu kuhusu nia yao ya kujitoa kwenye jumuiya hiyo.

Mapema Jumapili viongozi wa kijeshi walitangaza kwenye televisheni za taifa za Mali na Niger, na kuzua ufuatiliaji wa karibu miongoni mwa jumuiya ya kimataifa.

Baada ya mapinduzi ya kijeshi kutokea katika nchi hizo, ECOWAS, imeweka vikwazo vikali kwa nchi hizo tatu ili kushinikiza kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba, tangu majeshi yatwae madaraka kutoka kwa serikali za kiraia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha