Mali, Burkina Faso na Niger zatangaza kujiondoa kutoka kwenye ECOWAS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2024

Picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ikimuonyesha Kanali Abdoulaye Maiga, Waziri wa Uangalizi wa Mipaka na Ugatuaji Madaraka wa Mali, ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mpito ya Mali, akisoma taarifa ya pamoja kwenye kipindi cha taarifa ya habari cha televisheni ya Mali (ORTM), Januari 28, 2024. (Xinhua)

Picha ya skrini iliyochukuliwa kutoka kwenye video ikimuonyesha Kanali Abdoulaye Maiga, Waziri wa Uangalizi wa Mipaka na Ugatuaji Madaraka wa Mali, ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mpito ya Mali, akisoma taarifa ya pamoja kwenye kipindi cha taarifa ya habari cha televisheni ya Mali (ORTM), Januari 28, 2024. (Xinhua)

BAMAKO - Mali, Burkina Faso na Niger si nchi wanachama tena wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), maafisa wa kijeshi wa nchi hizo tatu wameamua katika taarifa ya pamoja iliyosomwa siku ya Jumapili kwenye kipindi cha taarifa ya habari cha televisheni ya Mali (ORTM).

Kwa upande wa Mali, taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imesomwa na Kanali Abdoulaye Maiga, Waziri wa Uangalizi wa Mipaka na Ugatuaji Madaraka wa Mali, ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mpito ya Mali.

Kwa mujibu wake, uamuzi huo umechukuliwa kwa "uhuru kamili" na Ibrahim Traore, Rais wa Mpito wa Burkina Faso, Kanali Assimi Goita, Rais wa mpito wa Mali, na Brigedia Jenerali Abdourahamane Tchiani, Rais wa Baraza la Taifa la Ulinzi wa Nchi ya Niger, wameamua kuchukua "wajibu wao mbele ya historia" kwa kuitikia "matarajio, wasiwasi na matumaini ya watu wao."

ECOWAS ilianzishwa Mwaka 1975 ikiwa na dhamira ya kuhimiza utandawazi wa uchumi katika nyanja zote za shughuli za kiuchumi, hasa viwanda, usafiri, mawasiliano ya simu, nishati, kilimo, maliasili, biashara, masuala ya kifedha, na masuala ya kijamii na kiutamaduni.

Ili kutaka nchi hizo tatu kurejesha utaratibu wa katiba, ECOWAS, yenye makao yake makuu Abuja, mji mkuu wa Nigeria, imeweka vikwazo vikali kwa nchi hizo tatu tangu majeshi ya nchi hizo yachukue mamlaka kwa kupindua serikali za kiraia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha