Michezo ya kwanza ya Kielektroniki ya Olimpiki itafanyika kabla ya Mwaka 2026: Rais wa IOC Bach

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2024

Washiriki wa Timu ya China wakishangilia baada ya fainali ya DOTA2 ya Michezo ya Kielektroniki (Esports) kwenye Michezo ya 19 ya Asia mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, China, Oktoba 2, 2023. (Xinhua/Yan Linyun)

GANGNEUNG, Korea Kusini - Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach amesema Jumatatu kwamba Mashindano ya kwanza ya Michezo ya Kielektroniki ya Olimpiki (e-sports) litatoka mapema mwaka ujao.

Kwenye Mkutano wa 141 cha IOC Oktoba mwaka jana, IOC ilitangaza mipango ya kuanzisha Michezo ya Kielektroniki ya Olimpiki (e-sports)

Bach amesema mpango huo bado haujawekwa kwa asilimia 100, lakini utafiti unaendelea na kupata maendeleo makubwa.

"Nadhani tunaweza kutarajia mashindano ya kwanza, kutoa Michezo ya Olimpiki ya Esports kama hii kwa mwaka 2025, au mapema 2026," Bach amesema.

IOC kujihusisha kwa mara ya kwanza na jamii ya esports ni katika kuandaa Baraza la Esports Mwaka 2018 huko Lausanne. Mwaka 2021, IOC ilitengeneza Michezo Mfululizo ya Mtandaoni ya Olimpiki, na kisha ikazindua Wiki ya Michezo ya Kielektroniki ya Olimpiki huko Singapore mwaka jana.

Bach amesema, kwa upande mmoja, kulikuwa na michezo ya mtandaoni inayomaanisha esports na shughuli za kimwili, na kwa upande mwingine, kulikuwa baadhi ya michezo maarufu ya kielektroniki inayoendana na maadili ya Olimpiki.

"Kwa hili, nadhani tunaweza kuweka pamoja mpango wa kuvutia sana lakini pia unaozingatia maadili," ameongeza.

Mapema siku hiyo, Bach alibainisha kuwa teknolojia za akili bandia (AI) zitachukua jukumu muhimu katika michezo na Michezo ya Olimpiki katika siku za usoni.

Washindi wa medali wakihudhuria hafla ya kukabidhi Mashindano ya kielekitroniki ya Peace Elite ya Michezo ya Asia katika Michezo ya 19 ya Asia, Oktoba 1, 2023. (Xinhua/Yan Linyun)

Washindi wa medali wakihudhuria hafla ya kukabidhi Mashindano ya kielekitroniki ya Peace Elite ya Michezo ya Asia katika Michezo ya 19 ya Asia, Oktoba 1, 2023. (Xinhua/Yan Linyun)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha