Hafla ya kuufungua tena Ubalozi wa China nchini Nauru yafanyika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 30, 2024

Luo Zhaohui (wa pili kulia), Mkuu wa  Idara ya Maendeleo na Ushirikiano ya Kimataifa ya China, ambaye ni mwakilishi wa serikali ya China   akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea (wa pili kushoto), wakifungua  bango lenye jina la ubalozi kwenye hafla ya kufunguliwa kwa ubalozi wa China nchini Nauru iliyofanyika kwenye hoteli moja nchini humo , Januari 29, 2024. (Picha na Chen Guolong/Xinhua)

Luo Zhaohui (wa pili kulia), Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano ya Kimataifa ya China, ambaye ni mwakilishi wa serikali ya China akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea (wa pili kushoto), wakifungua bango lenye jina la ubalozi kwenye hafla ya kufunguliwa kwa ubalozi wa China nchini Nauru iliyofanyika kwenye hoteli moja nchini humo, Januari 29, 2024. (Picha na Chen Guolong/Xinhua)

YAREN – Hafla ya kufunguliwa tena kwa ubalozi wa China nchini Nauru imefanyika Jumatatu jioni katika hoteli iliyo kusini mashariki mwa nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari ya Pasifiki, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea na mwakilishi wa serikali ya China Bw.Luo Zhaohui, Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano ya Kimataifa ya China wameshiriki kwenye hafla hiyo.

Aingimea amesema katika hotuba yake kwenye hafla hiyo kwamba kuendeleza uhusiano na China kunakaribishwa sana nchini Nauru. "Nauru inatazamia kile tunachoweza kufanya pamoja," amesema.

Wang Xuguang, mkuu wa ujumbe wenye wajibu wa kujenga upya ubalozi wa China nchini Nauru, amesema katika hotuba yake kwamba kutambua kanuni ya kuwepo kwa China moja ndiyo msingi wa kisiasa wa kurejesha na kuendeleza uhusiano wa pande mbili.

"Kuanzia mwanzo huu mpya, nchi hizi mbili zitaendelea kuaminiana kisiasa, kuungana mkono katika kutafuta kwa kujiamulia njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi, kushughulikia maslahi na mambo makuu ya kila upande wao, kuungana mkono na kushirikiana kwa karibu katika masuala ya kimataifa na kikanda, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kwenye kilele kipya," Wang amesema.

Marcus Stephen, Spika wa Bunge la Nauru, na maafisa wengine wa serikali na bunge la Nauru, pamoja na wajumbe wa kampuni ya China na jamii ya Wachina wanaoishi Nauru pia walishiriki kwenye hafla hiyo.

Hafla ya kupandisha bendera ya Taifa la China ilifanyika mapema Jumatatu asubuhi huko Nauru na ujumbe wa wanadiplomasia wa China, ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka 19 iliyopita bendera nyekundu ya nyota tano imepeperushwa tena katika kisiwa hicho.

China na Nauru zilitia saini taarifa ya pamoja mjini Beijing Januari 24 kuhusu kurudishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kwenye ngazi ya kibalozi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea akizungumza kwenye hafla ya kufunguliwa tena kwa ubalozi wa China nchini Nauru iliyofanyika katika hoteli moja nchini humo , Januari 29, 2024. (Picha na Chen Guolong/Xinhua)

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Nauru Lionel Aingimea akizungumza kwenye hafla ya kufunguliwa tena kwa ubalozi wa China nchini Nauru iliyofanyika katika hoteli moja nchini humo, Januari 29, 2024. (Picha na Chen Guolong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha