

Lugha Nyingine
Mtafiti wa Afrika atoa wito wa kurekebishwa kwa mifumo ya afya ya kudhibiti janga wakati matishio yakiongezeka
Mchambuzi mkuu wa utafiti na sera wa Taasisi ya Afrika ya Sera ya Maendeleo (AFIDEP) Bw. Michael Chipeta, amesema mifumo ya huduma za afya barani Afrika inapaswa kurekebishwa, ili kuhakikisha kuwa inahimili zaidi matishio ya majanga katika siku zijazo, yanayohusiana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa makazi.
Bw. Chipeta amesema janga la COVID-19 lilifichua udhaifu wa miundombinu ya huduma za afya barani Afrika, na hivyo kuna haja ya kuipanga upya na kuhakikisha kwamba haitatetereka kutokana na milipuko isiyotarajiwa.
Ameongeza kuwa ingawa Bara la Afrika limeepushwa na athari mbaya zaidi ya janga hilo, serikali zinapaswa kuweka kipaumbele cha uwekezaji katika tahadhari za mapema, utambuzi, dawa muhimu, na ushiriki wa jamii katika kusaidia kukabiliana na majanga ya siku zijazo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma