

Lugha Nyingine
Ushirikiano kati ya China na Zimbabwe waboresha maendeleo ya rasilimali watu
Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Zimbabwe Mercy Dinha akiongea kwenye hafla ya ushirikiano wa maendeleo ya rasilimali watu kati ya China na Zimbabwe iliyofanyika katika Ubalozi wa China nchini Zimbabwe huko Harare, Januari 29, 2024. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)
Maofisa wa serikali ya Zimbabwe wamesema ushirikiano kati ya China na Zimbabwe katika kujenga uwezo wa watu umeimarisha maendeleo ya rasilimali watu nchini Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Zimbabwe Bibi Mercy Dinha, amesema matunda ya ushirikiano huu yamekuwa mengi, na kuhimiza maendeleo ya maofisa na wataalamu ambao wamechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi yao.
Bibi Dinha amesema hayo kwenye hafla ya ushirikiano wa maendeleo ya rasilimali watu kati ya China na Zimbabwe iliyofanyika kwenye Ubalozi wa China mjini Harare.
Amesema historia ya miongo mingi ya ushiriki wa China katika maendeleo ya rasilimali watu nchini Zimbabwe, inaonyesha kwa kina kujitoa kwa China katika kuzipatia nchi zinazoendelea ujuzi, utaalamu na rasilimali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma