

Lugha Nyingine
Tanzania na China zasaini mkataba kwa ajili ya mradi wa eneo la jiolojia la Ngorongoro-Lengai
(CRI Online) Januari 30, 2024
Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesaini makubaliano na serikali ya China yakilenga kuendelea na utekelezaji wa mradi wa eneo la jiolojia la Ngorongoro-Lengai.
Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita imesema kwamba mradi huo, wenye thamani ya shilingi bilioni 25, umesainiwa na kamishna wa NCAA, Richard Kiiza na kaimu balozi wa China nchini Tanzania Chu Kun.
Mradi huo utajumuisha ujenzi wa miundo mbinu ya utalii na unatarajiwa kukamilika Juni 2025.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma