

Lugha Nyingine
China yampongeza Bw. Azali Assoumani kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Comoro
(CRI Online) Januari 30, 2024
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, China inampongeza Bw. Azali Assoumani kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine.
Msemaji huyo amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa Rais Assoumani, Comoro itapata mafanikio makubwa zaidi kwenye ujenzi wa taifa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
China siku zote inatilia maanani kukuza uhusiano wa kirafiki na Comoro na inapenda kufanya jitihada pamoja na serikali mpya ya nchi hiyo katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na kutoa msukumo mpya katika maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma