Rais Xi apokea nyaraka za utambulisho wa taifa za mabalozi wapya nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2024

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea  nyaraka za utambulisho wa taifa za mabalozi wapya 42 nchini China  katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amepokea nyaraka za utambulisho wa taifa za mabalozi wapya 42 nchini China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing Jumanne alasiri ambapo amewataka mabalozi hao kufikisha salamu zake za kutakia kila la kheri na kuombea mema kwa viongozi wa nchi zao na watu wote. Mabalozi hao wanatoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo Kenya, Tanzania, Zambia, Ukraine, Afghanistan na Japan.

Katika hotuba yake baada ya hafla hiyo, Rais Xi amesema, China inathamini urafiki na watu wa nchi mbalimbali, China ingependa kuzidisha urafiki na kupanua ushirikiano wa kunufaishana na watu wa nchi mbalimbali kwenye msingi wa kuwa na usawa na kunufaishana, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili mbili. Na inatumai mabalozi wataijua China kwa pande zote na kwa kina, na kusaidia kuimarisha ukaribu wa ushirikiano na kujenga daraja la mawasiliano kwa ajili ya uhusiano wa pande mbili mbili. Serikali ya China itatoa uungaji mkono na urahisi kwa mabalozi hao katika utekelezaji wa majukumu yao.

Rais Xi amesisitiza kuwa "Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China," China inaendeleza kwa pande zote ujenzi wa nchi yenye nguvu na ujenzi wa mambo makubwa ya ustawishaji wa taifa kwa kupitia maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Amesema, dhamira na madhumuni ya maendeleo ya mambo ya kisasa ya China ni kuwezesha Wachina zaidi ya bilioni 1.4 kuishi maisha bora, na kwamba kwa Dunia, hii inamaanisha soko pana na fursa za maendeleo ambazo hazijawahi kutokea, ambazo zitaleta msukumo mkubwa katika maendeleo ya mambo ya kisasa kwa nchi duniani kote.

Amesema hali ya sasa ya Dunia siyo ya amani. Kwa kutilia maanani mustakabali wa binadamu na ustawi wa watu wake, China, kama ilivyofanya siku zote zilizopita, itajitahidi kuchangia hekima na mapendekezo yake kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu, kutetea Dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi ambao ni wa jumuishi na wenye manufaa kwa wote, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kushirikiana kuijenga Dunia iwe nzuri zaidi.

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea  nyaraka za utambulisho wa taifa za mabalozi wapya 42 nchini China  katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba baada ya kupokea  nyaraka za utambulisho wa taifa za mabalozi wapya 42 nchini China  katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha