Rais Xi Jinping ampongeza Bw. Azali Assoumani kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine

(CRI Online) Januari 31, 2024

Rais Xi Jinping wa China Januari 28 alizungumza kwa njia ya simu na Bw. Azali Assoumani, akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Comoro kwa muhula mwingine.

Rais Xi amesema China na Comoro ni marafiki wakubwa, wenzi na ndugu wazuri wenye urafiki na kuaminiana kwa dhati.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepiga hatua kwa kasi na ushirikiano wenye matokeo halisi kati ya pande hizo mbili umezaa matunda kwenye nyanja mbalimbali, Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa, China na Comoro zimekuwa zikiungana mkono kithabiti kwenye masuala yanayohusiana na maslahi ya upande mwingine na yale yanayofuatiliwa na upande mwingine.

Rais Xi amesema anatilia maanani sana uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na yuko tayari kushirikiana na Rais Assoumani katika kusukuma mbele uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi ya juu zaidi na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha