China itaongeza ushirikiano na UN ili kuhimiza usimamizi wa dunia nzima uwe wa haki na halali zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2024

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na   mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mjini Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mjini Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na mwenyekiti wa Baraza Kuu 78 la Umoja wa Mataifa Dennis Francis siku ya Jumanne mjini Beijing akisema kuwa ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China siku zote imekuwa ikitekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi na kulinda heshima na maamuzi na hadhi ya Umoja wa Mataifa (UN).

Ameongeza kuwa China inatetea Dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu na utandawazi wa kiuchumi unaonufaisha wote, na inahimiza nchi zote kushirikiana ili kukabiliana na changamoto na kufikia ustawi kwa pamoja.

Han amesema kuwa Mwaka 2025 ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, China ingependa kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa na kuungana mkono na pande zote kufanya kazi kwa ajili ya kuhimiza mfumo wa usimamizi wa dunia nzima uwe wa haki na halali zaidi chini ya mwongozo wa dhana ya ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Akiita China kuwa mshirika mwenza wa Umoja wa Mataifa na nguvu thabiti katika kulinda amani na maendeleo ya Dunia, mwenyekiti Francis amesema China inatarajiwa kufanya kazi muhimu zaidi katika kuhimiza maendeleo endelevu, ushirikiano wa kimataifa na kukabiliana na changamoto za dunia nzima.

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na   mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mjini Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mjini Beijing, China, Januari 30, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha