Marekani yarejesha vikwazo kwa Venezuela kufuatia Venezuela kupiga marufuku kwa mgombea wa upinzani kuwania urais

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 31, 2024

Magari yakiendeshwa kwenye barabara kuu mjini Caracas, Venezuela, Julai 20, 2021. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)

Magari yakiendeshwa kwenye barabara kuu mjini Caracas, Venezuela, Julai 20, 2021. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)

WASHINGTON - Serikali ya Joe Biden imeiwekea tena vikwazo Venezuela vinavyolenga sekta yake ya mafuta na gesi siku ya Jumanne, ikisema kuwa hatua hiyo ni kujibu uamuzi wa serikali ya Venezuela kupiga marufuku mgombea mkuu wa upinzani kuwania urais.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller amesema katika taarifa yake kwamba kwa vile serikali ya Maduro imeshindwa kuheshimu makubaliano iliyoafikiwa Mwezi Oktoba na Muungano wa upinzani wa Unitary Platform ya kuruhusu wagombea wote wa upinzani kushiriki katika uchaguzi wa urais baadaye mwaka huu, Marekani haitaongeza muda wa msaada kwa sekta ya mafuta na gesi ya Venezuela baada ya tarehe yake ya mwisho ya Aprili 18.

msaada huo unaojulikana kwa jina la Leseni ya Jumla Namba 44, ulitolewa mwezi Oktoba ili kuhimiza serikali ya Maduro kutekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa huko Barbados.

Zaidi ya hayo, Marekani inafuta Leseni ya Jumla Namba 43, ambayo inaidhinisha biashara kati ya watu wa Marekani na Minerven, kampuni ya uchimbaji dhahabu inayomilikiwa na serikali ya Venezuela.

Mahakama ya Juu ya Venezuela siku ya Ijumaa iliidhinisha marufuku inayomzuia mgombea urais wa upinzani nchini humo Maria Corina Machado kushikilia wadhifa wa umma.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kurejeshwa kwa vikwazo hivyo Jumatatu, John Kirby, mratibu wa mawasiliano ya kimkakati katika Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani, ameuambia mkutano na waandishi wa habari ya Ikulu ya Marekani kwamba, Maduro na washirika wake "hawajachukua hatua hizo" walizoahidi kuzitekeleza kwenye Makubaliano ya Barbados.

"Sasa, wanao muda hadi Aprili kufanya hivyo, kwa hivyo tuna machaguo yaliyopo kwetu. Sitadurusu yoyote kati ya hayo kwa wakati huu. Lakini kwa hakika tuna machaguo, kuhusiana na vikwazo na kitu kama hicho ambavyo tunaweza kuchukua," Kirby amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha