

Lugha Nyingine
Tanzania yajipanga kuifanyia mageuzi tasnia ya Ubunifu
(CRI Online) Januari 31, 2024
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya nchini Tanzania imesema, wadau 800 wa utamaduni na sanaa nchini humo wanatarajiwa kukutana mwezi ujao kujadili masuala yanayoathiri tasnia hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gerson Msigwa, amewaambia wanahabari siku ya Jumanne kuwa, mkutano huo unalenga kukutanisha wadau muhimu wa sekta hiyo watakaojadili masuala na changamoto zao, kujenga mtandao, na kubadilishana uzoefu ili kuifanya sekta hiyo iendelee kusonga mbele.
Aidha, Msigwa amesema, katika mkutano huo watajadili hali ya sekta ya utamaduni na Sanaa nchini humo na kutoa mapendekezo ya maboresho, kujadili changamoto na mikakati ya kuzitatua changamoto hizo, na kutambua na kuwazawadia wadau waliofanya vizuri katika sekta hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma