Burkina Faso yasema imejiandaa kwa matokeo ya kujitoa ECOWAS

(CRI Online) Januari 31, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Diaspora wa Burkina Faso, Karamoko Jean Marie Traore amesema, nchi hiyo itafanya kazi kupunguza matokeo hasi ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Akizungumzia matokeo ya hatua hiyo kupitia kituo cha televisheni cha taifa cha nchi hiyo, RTB, Bw. Karamoko amesema, ushirikiano na nchi wanachama wengine wa ECOWAS unajumuisha maeneo mbalimbali.

Jumapili iliyopita, Mali, Burkina Faso, na Niger zilitoa taarifa ya pamoja kuhusu kujitoa ECOWAS, jumuiya ya kikanda yenye nchi wanachama 15.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha