Chama cha Kikomunisti cha China chapongezwa kwa sera za kuwajali watu wa chini

(CRI Online) Februari 01, 2024

Chama cha kikomunisti cha Kenya (CPK) kimepongeza mchango wa China katika kuliinua Bara la Afrika na kwa kujali watu wa chini nchini mwake.

Pongezi hizo zinakuja miezi michache tu baada ya chama hicho kutuma ujumbe nchini China na kufanya mabadilishano na viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu sera bora za kuinua watu kiuchumi.

Akizungumza na Radio China Kimataifa, katibu mkuu wa Chama hicho Bw. Booker Ngesa Omole amesema China imefanikiwa kutokomeza umaskini na kuboresha sekta za elimu na kilimo ambazo ni tegemeo kuu la watu wa chini. Amezitaka nchi za Afrika kuiga mfano wa China ili kuinua maisha ya wengi barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha