

Lugha Nyingine
China yaendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo
BEIJING - China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara barani Afrika kwa miaka 15 mfululizo, huku thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ikifikia rekodi ya dola za Marekani bilioni 282.1 Mwaka 2023, Ofisa wa Wizara ya Biashara ya China Jiang Wei amesema Jumatano.
"Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ndiyo msingi na kichocheo cha uhusiano kati ya China na Afrika," Jiang amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Amesema kuwa, Baraza la Serikali la China limeidhinisha mpango wa jumla wa kujenga eneo la majaribio la ushirikiano wa kina wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.
Kwa mujibu wa mpango huo, China itaanzisha eneo la majaribio kama jukwaa la ufunguaji mlango na kushirikiana na Afrika ambalo litakuwa na nguvu fulani ya ushawishi wa kimataifa ifikapo Mwaka 2027.
"Lengo kuu ni kujenga jukwaa lenye ushindani wa kimataifa la ushirikiano na Afrika," Jiang amesema.
Katika miaka ijayo, pande hizo mbili zitalifanya eneo hilo la majaribio lioneshe vya kutosha umuhimu wake wa kuongoza, kuhimiza kazi ya kubadilisha muundo wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili, na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa China na Afrika, amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma