Ethiopia yazuia mashambulizi 4,550 ya mtandaoni ndani ya miezi sita

(CRI Online) Februari 01, 2024

Ethiopia imezuia mashambulizi zaidi ya 4,550 ya mtandaoni ndani ya miezi sita ya kwanza katika mwaka wa fedha wa 2023/24, ulioanzia Julai mwaka jana.

Katibu Mkuu wa Mamlaka ya Usalama wa Mtandao nchini Ethiopia (INSA), Bw. Solomon Soka amesema mamlaka yake imefanikiwa kuzuia asilimia zaidi ya 98 ya mashambulizi yote 4,623 ya mtandaoni dhidi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ofisa huyu mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Ethiopia yameongezeka kwa asilimia 115 kuliko mwaka uliopita wa fedha, hali inayochangiwa na matumizi mapana ya teknolojia ya kidijitali duniani, kuongezeka kwa faida wanazopata washambuliaji, na maendeleo ya kasi ya miundombinu ya kidijitali nchini Ethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha