Madaktari wa China wa mishipa ya fahamu wawasili Dar es Salaam kwa Mpango wa mwaka mmoja

(CRI Online) Februari 01, 2024

Jumla ya madaktari 11 wa magonjwa ya mishipa ya fahamu kutoka China wamewasili nchini Tanzania tayari kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa muda wa mwaka mmoja katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa MOI, Dk. Lemeri Mchome amesisitiza kuwa ujio wa madaktari hao unatoa fursa muhimu kwa wataalamu wa nchini humo kujifunza kutoka kwa wenzao wa China.

Mpango huo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China.

"Wenzetu wa China wamepiga hatua kubwa katika matibabu ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu... Ninaamini kwamba hadi watakapoondoka, tutakuwa tumeboresha sana uwezo wetu," amesema Dk. Mchome.

Mbali na MOI, wataalamu hao pia watatoa huduma zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), na Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha