Daraja kubwa lenye umbo la upinde katika Mkoa wa Guangxi wa China lazinduliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 02, 2024

Picha iliyopigwa Januari 31, 2024 ikionyesha Daraja la Tian'e Longtan katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Januari 31, 2024 ikionyesha Daraja la Tian'e Longtan katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

NANNING - Daraja la Tian'e Longtan, ambalo ni daraja lililojengwa kwa zege na kuimarishwa kwa chuma lenye urefu wa mita zaidi ya 600 kwenda juu, limezinduliwa siku ya Alhamisi katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China.

Daraja hilo lililo juu ya Mto Hongshui, ambalo liko katika Wilaya ya Tian'e ya Mji wa Hechi wa Guangxi, ni daraja lenye barabara mbili zenye njia nne za kupitisha magari likiwa na urefu wa mita jumla ya 2,488.55. Ni daraja refu zaidi duniani kwa ukubwa lenye umbo la upinde lililojengwa kwa zege na kuimarishwa kwa chuma.

Kufunguliwa kwa Daraja la Tian'e Longtan kunaonesha kukamilika kwa ujenzi wa Barabara Kuu ya Nantian inayounganisha wilaya za Nandan na Tian'e za Guangxi, na kupunguza muda wa safari kutoka mwendo wa saa 1.5 hadi dakika 40 kwa gari. Ujenzi wa muundo mkuu wa daraja hilo ulianza Desemba 2020.

Kukamilika kwa ujenzi wa Daraja hilo la Tian'e Longtan ni hatua muhimu katika mchakato wa ujenzi wa madaraja yenye umbo la upinde.

Changamoto nyingi zilitatuliwa na uvumbuzi kufikiwa wakati wa ujenzi wa daraja hilo, na kutengeneza njia kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya madaraja ya zege yenye umbo la upinde, hasa matumizi yake kwenye barabara kuu na reli za milimani, amesema Zheng Jielian, mtaalamu mkuu wa Taasisi kuu ya Uhandisi ya China. 

Picha iliyopigwa Januari 31, 2024 ikionyesha Daraja la Tian'e Longtan katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Januari 31, 2024 ikionyesha Daraja la Tian'e Longtan katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha